Song: Tumekubalika
Artist: Ambwene Mwasongwe
Chorus
Tumekubalika na Mungu tuna nguvu za ki-falme
Ametuchora kweli moyoni mwake tu uzao wa agano 2
Tu uzao mteule aaah aaaaah aaah
Ukuhani wa ki-falmee eeeh aaah aaah
Taifa takatifu aaah aaah oooh ooh
Watu wa milki ya Mungu aaah aaah oooh oh
VERSE
Nimemwona Mungu amewaleta kutoka
Misri wana nguvu kama za nyati watawavunja adui mifupa
vipande vipande watawachoma adui kwa mishale
yeye kawabariki nani aawalaani, Mungu kawabariki
nani wakuwapinga wana nguvuu aaah Mungu kawapa aaah
wanaweza aaah BWANA kawapa aaah........OOOH
Wanautishoo aaah BWANA kawapa aaah oooh oooh
Hatuwezi tishwa kwa maneno yao nguvu zetu zipo
kwa Bwana aaah tulipona kwa Farao
Tukiwa ugenini hatukufa kwa njaa tukiwa hatuna kitu,
Tulinusurika vita tukiwa hatuna silaha, tulipona magonjwa
Tukiwa hatuna dawa tulipona ma-wifi ndoa zikiwa tetee
Tuliweza maisha tukiwa hatuna hela, tulishinda upweke
Tukiwa tumeachwa tuliponywa kesi bila ya mtetezi
Mungu alikuwepo hatukuwa pekee yetu waliotuonea hilo
hawakuja katutoa Misri tuna nguvu kama za nyati kuvunja vipande,
katutoa Misri tuna nguvu kama za nyati kuvunja vipande yayaah yaah
TUMEKUBALIKA
Chorus
Tumekubalika na Mungu
Tuna nguvu za ki-falme ametuchora
kweli moyoni mwake tu uzao wa agano 2
Usiye lala aaah aah
Usiye lala aaaah aaah
Usiye lala aah aaah aaah
Usiye lala AAAA AAAAH
VERSE
Usiwachokoze walio na Mungu wamebarikiwa na
Mungu wakitupwa jangwani wateseke wafe huligeuza bustanii
Tulikula mtama kwa maji tukanawiri kuliko wao hatukupambwa
kama wao tukapendeza zaidi yao, walitubadilisha majina hawakubadili
Hatima walipotutupa shimoni tukaibukia IKULU, kule walipotusukumia
ndiko Mungu hupumzikia, walidhani wanatukimbiza kumbe
WANATUSINDIKIZA
Bwana wangu ..........' YESU
YESUU YESU
Shindii ................... YESU
Mwamba......... YESU
weweeh ..... YESU
aaah haaaaaaa aah
Jiwe langu YESU
Ngome YESU
Mwambaaa aaah
Bwana YESU
Oooh uuuh
Jiwe langu YESU
Mwaminifu YESU
Haki YESU
nguzo YESU
Jina lako YESU
Haki YESU
Mwaminifu YESU
Weweeee aaaaaah aaaaah
Chorus
Tumekubalika na Mungu
Tuna nguvu za kifalme ametuchora
kweli moyoni mwake tu zao wa agano 2