Sunday, January 28, 2018

KIJANA BADILI FIKRA NA MATAZAMO WAKO

KUCHEZA BAHATI NASIBU NI  UVIVU WA KUFIKIRIA..!

Mtu yeyote unayemuona amefanikiwa katika nafasi fulani ya maisha ,ujue si Kwa bahat Mbaya au Nzuri iliyomfanya awe hivyo unavyomuona Leo Bali ni kwa MAKUSUDI.

Kwa kujitambua Yeye ni nani, wapi alipo Sasa, Ni wapi anataka kuwepo Kesho na njia gani atumie Ili afike pale anapotaka kufika.

Na kikubwa kwenye maisha ni kuwa na
, maana mafanikio ni jambo la mchakato unaokutoa sehemu moja kwenda nyingine kidogo kidogo hatimaye unajikuta Umefika ulipopataka.

Lakini vijana wengi wa Sasa wanafikiri kufanikiwa ni jambo linalopatikana #instant yaan kufamba na kufumbua, leo alale masikini Kesho aamke Tajiri wanaishi kwa matumaini na si Kwa MAKUSUDI

Ndio maana Miaka ya hivi Karibuni kumekuwa na wimbi Kubwa Sana la michezo ya Kubashiri(ku Bet), droo za bahati nasibu nk, Sehemu Kubwa ya matangazo kwa Sasa kwenye vyombo vya Habari ni matangazo yanayohusu BAHATI NASIBU na vijana ambao wenye Nguvu wanaotegemewa kuleta mabadiliko ya kiuchumi ndio wadau wakubwa wa michezo hiyo, Ina nihuzunisha kwa kweli.

Vijana wengi ni WAVIVU si tu wa kufanya kazi Bali pia kufikiria, wengi walitegemea KUAJIRIWA na pale Ajira zinapoonekana kuwa ngumu hawana PLAN B ya nini wanatakiwa wafanye, Jibu lao La mwisho kwa Sasa ni kushinda na Simu zao viganjani wakifanya mihamala kwenye makampuni ya bahat nasibu, labda siku moja watabahatika kupokea mamilioni ya PESA pale watakapotangazwa kuwa washindi.

Na labda wengi hawafahamu, wanaotajirika na michezo Hiyo si mwananchi mmoja mmoja anayecheza Bali ni makampuni hayo ya bahati nasibu, ebu fikiria ni watanzania wanagapi wanacheza kila siku kwa kutoa pesa zao na ni sh ngapi wanaingiza kutoka kwa watanzania wanaosema maisha magumu kujitajirisha?  na kumbuka  anayebahatika kuwa mshindi ni mtu mmoja au wawili kwa wiki au mwezi.

Sasa kama Wanaocheza tuseme ni milioni moja kwa siku na mshindi ni mtu mmoja Tu kati ya hao,anayepatikana baada ya wiki, bado unasubiria foleni yako na wewe utangazwe kuwa mshindi kati ya hao? Unaweza ukajikuta umezeeka na hujatangazwa kuwa mshindi.

Hivi ni kweli ukomo wetu wa AKILI Umefika Mwisho Hapo kucheza bahati nasibu❓ Ukishindwa KUFIKIRI basi watu Wengine WATAFIKIRI kwa ajili yako.

RAFIKI_AMKA

MAFANIKIO HAYAJI MARA MOJA.

..........................

Mzalendo

John C Ntogwisangu

Watsap 0712463344.

Kwa mtini jifunzeni #
Blogger: Vicent Mathias
Phone: 0755 042 030.

1 comment:

TUMEKUBALIKA By: Ambwene Mwasongwe lyrics.

Song : Tumekubalika Artist : Ambwene Mwasongwe Chorus Tumekubalika na Mungu tuna nguvu za ki-falme Ametuchora kweli moyoni mwake tu uz...