Sunday, January 28, 2018

KUWA NA YESU KRISTO

MAMBO MUHIMU
Mambo muhimu matano (5) ya kufanya au kuwa nayo ili kukua kiroho.

1. Kumpokea Yesu kama BWANA na Mwokozi wa maisha yako pamoja na kujazwa Roho Mtakatifu.
Yohana 1:12-13
Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.

2. Kuwa na Moyo safi
Mathayo 5:8 Heri wenye moyo safi;
Maana hao watamwona Mungu.
pia unaweza kusoma katika Zaburi 33:1

3. Kudumu katika Neno la Mungu.
Wakolosai 3:16-17 Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.

4. Ambatana na watu wenye imani moja sawa na wewe
2 Mambo ya Nyakati 15:2;.......... BWANA yu pamoja nanyi, mkiwa pamoja naye; nanyi mkimtafuta ataonekana kwenu; lakini mkimwacha atawaacha ninyi.  2 Timotheo 2:22 Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.

5. Punguza marafiki
Mithali 18:24 Ajifanyiaye rafiki wengi ni kwa uangamivu wake mwenyewe;
Lakini yuko rafiki aambatanaye na mtu kuliko ndugu.

Kwa Mtini Jifunzeni#
Blogger: Vicent Mathias
Phone: 0755 042 030.

1 comment:

  1. MUNGU AWABARIKI SANA.
    SHARE KWA WAPENDWA WAKO NAO PIA WABARIKIWE KWA UJUMBE HUU MFUPI.

    ReplyDelete

TUMEKUBALIKA By: Ambwene Mwasongwe lyrics.

Song : Tumekubalika Artist : Ambwene Mwasongwe Chorus Tumekubalika na Mungu tuna nguvu za ki-falme Ametuchora kweli moyoni mwake tu uz...